CLUB TAJIRI ZA SOKA DUNIANI KWA SASA NDIO HIZI.


                               

KLABU ya Manchester United imerejea kwenye nafasi ya kwanza kwa utajiri miongoni mwa klabu za soka duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
United hivi sasa inaelezwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 2.24 baada ya kutoa ripoti yake kufuatia fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Real Madrid inashika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola za KImarekani Bilioni 1.88, ambayo ni sawa na kupanda kwa asilimia kwa 29, wakati mabingwa wa Ulaya na Hispania, Barcelona wanashika nafasi ya tatu wakiwa na utajiri wa dola Bilioni 1.31, sawa na ongezeko la asilimia 34.
Tano bora inakamilishwa na Bayern Munich na Arsenal na Forbes limebashiri kwamba kwa asili ya Ligi ya Mabingwa, tajiri atazidi kuwa tajiri.
Manchester United ina dola Milioni 192 zaidi ya New York Yankees na Dallas Cowboys.

Categories: