HII NDIO MELI YA MAGUFULI INAYOZAMA.


ILE meli maarufu ijulikanayo kama ‘Meli ya Magufuli’ ambayo Serikali ya Tanzania iliinasa katika Eneo lake la bahari ya hindi ikivua samaki bila Kibali, imeanza kuzama baharini baada ya kuharibika vibaya.
Meli hiyo ya Tawaliq 1 ilikamatwa ikiwa na wavuvi 34 na hadi kufikia mwisho wa Kesi hiyo jumla ya wavuvi 20 walitiwa hatiani Lakini licha ya Mahakama kuamuru meli hiyo itaifishwe kwa sababu ilikuwa haijulikani na Tume inayojihusisha na shughuli za uvuvi katika Bahari ya India (IOCT), meli hiyo imeanza kuzama kama inavyoonekana kwenye picha ambapo sababu ni kutoboka baadhi ya maeneo hivyo kuingiza maji ndani.Categories: