Busta Rhymes Fans: Hii Niyenu tena.


Busta Rhymes ana mpango wa kutoa Album yake nyingine inayofahamika kama YEAR OF THE DRAGON ambayo itapatikana kwenye Google Play BURE. Kwa mujibu wa maneno yake, album hii haihusiani na Cash Money ila itamshirikisha kiongozi wake Lil Wayne. Akiweka msisitizo, Busta Rhymes a.k.a King Tut alisema, "Hii ni Album yangu ya Google, na atapewa kila mtu bure".
Busta Rhymes aliendelea mwaga info akisema, "Sababu iliyotufanya tuamue kumpa kila mtu bure ni moja, Google Play ni mahali ambapo itapatikana. Hivyo ikitoka, ambayo ni wiki ya pili ya Agosti na utapata tarehe husika siku chache zijazo. Ni muhimu kwenda na kuipata huko kwa sababu ndio sehemu pekee utakapoipata BURE " alisema King Tut.
Zaidi ya Lil Wayne, album hii pia itamshirikisha MMG Boss Rick Ross na wengine wengi. " Tuna Tunechi, tuna RickRossRobin Thicke, Maino and Anthony Hamilton kwenye wimbo pamoja, Gucci Mane, tuna Reek Villain na J-Doe", alisema Busta kwenye 106 & PARK.

Categories: