MwanaFA, Madtraxx, Bamboo. Kwenye Nokia Don’t Break the Beat(final)

Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA anatarajiwa kutumbuiza kwenye fanaili za shindano la freestyle la kampuni ya simu Nokia liitwalo Nokia Don’t Break the Beat.Fainali hizo zitafanyika Jumamosi September 1 jijini Nairobi, Kenya katika Club Ichonic saa 2 usiku.wasanii wengine watakao kuwepo ni Bamboo, Keko, Madtraxx, Octopizzo na STL.
Mshindi wa kwanza kwenye shindano hilo atajishindia 5 million pamoja na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Decimal Media/Universal Records kwa kurekodi nyimbo pamoja na video.
Tangu mwezi uliopita msako wa kumpata mkali wa michano Afrika Mashariki umeendelea kwa kuzunguka kwenye miji ya Mombasa, Nairobi, Kampala, Dar-es-Salaam, Kisumu, na Eldoret .