AY Sasa ni Official Airtel Ambassador


AY
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemtangaza Msanii AY kuwa Balozi wake mpya kwa mwaka 2012-2013 ikiwa ni utaratibu iliyojiwekea katika kushirikiana na wasanii nchini ili kufanyashughuli mbalimbali za kijamii.

Akiongea na
waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa Airtel JacksonMmbando alisema “Airtel tumeingia makubaliano na msanii AY kuwa Balozi wetu wa mwaka huu, lengo letu ni kuendelea kuwa karibu zaidi na wasanii wetu nchini na pia kufanya nao shughuli za kijamii ili kufaidisha taifa letu kwa kuwa wasanii wetu ni mahiri zaidi nawote tunafahamu AY ni msanii mkongwe na anayejituma, hivyo tunaamini ushirikiano huu utaweza kutimiza malengo yetu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhudumia jamii kupitia miradi mbali mbali ya jamii inayoendeshwa na Airtel pamoja na kuiwakilisha Airtel kwa kuwa Balozi mzuri”

Kwa upande wake Ambwene Yessayah kama balozi wa Airtel alisema “kwa kushirikiana na Airtel nitakuwa nikifanya shughuli za kijamii, hususani katika kuchangia ukuaji wa Elimu nchini. Pamoja na Airtel tutashirikisha vyombo na taasis nyingine ikiwemo vyombo mbalimbali vya Habari ili kuweza kufanikisha yote hayo. Kwa Kushirikiana na Airtel tutaandaa maonyesho mbalimbali ya burudani kwa ajili ya wateja wetu na hii itatangazwa hivi karibuni”

Categories: , ,