Chris Brown ampiga chini mpenzi wake Karrueche sababu ya Rihanna


Chris Brown amesema ameachana rasmi na mpenzi wake Karrueche Tran kwa maelezo kuwa hapendi kumuona akiumia kutokana na urafiki wake na Rihanna.
Brown ametoa taarifa hiyo kwa kusema "I have decided to be single to focus on my career. I love Karrueche very much but I don't want to see her hurt over my friendship with Rihanna," Chris Brown tells Confidenti@l through his spokesman on Thursday. "I'd rather be single allowing us to be both be happy in our lives."


Tangazo hilo la Chris Brown limekuja baada ya Brown na Rihanna kuonekana pamoja kwenye show ya Jay Z huko Brooklyn juzi usiku.
Hata hivyo Karrueche amedaiwa kutoiamini kauli ya Chris kuwa ni rafiki tu na Rihanna na amewaambia marafiki zake kuwa anaamini wawili hao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Mtandao wa TMZ umesema kuwa Karrueche anaona amesalitiwa na mpenzi wake huyo kwakuwa alimwahidi kuwa yeye ndio mwanamke pekee katika maisha yake baada ya kutaka kujua msimamo wake juu ya Rihanna.
Umesema Karrueche alikuwa ameshachezwa ‘machale’ kuwa wapenzi hao wa zamani walikuwa wakimzunguka kwakuwa wiki mbili zilizopita Chris alikuwa amebadilika kwa kwenda klabu peke yake na kumkwepa mpenzi wake.
Vyanzo vimeuambia mtandao huo kuwa Karrueche aliwaambia marafiki zake kuwa alimpenda Chris kwa dhati na alihisi uhusiano ulikuwa imara mpaka pale Rihanna aliporudi tena kwenye picha.