Jokate Azindua rasmi kampuni yake ya Kidoti Loving >>>>(pics)


Mrembo wa nchi Tanzania Jokate Mwegelo leo ameizundua rasmi kampuni yake ya Kidoti Loving katika hafla iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Bidhaa za kwanza za Kidoti zilizoingia sokoni ni Nywele (weaving) ambazo amesema tayari zinapatikana katika soko la Kariakoo na maeneo mengine jijini Dar es Salaam ambapo baada ya muda mfupi zitaanza kupatikana mikoani.
Amesema kwa kuanzia kampuni yake imeanza kwa kutengeneza nywele za aina nane ambazo zinapatikama kwa bei ya kawaida ili kuwawezesha watanzania wengi kupendeza kwa gharama nafuu.
Jokate alisema:-
“Hizi nywele mabibi na mabwana zimefanyiwa utafiti kwa takriban mwaka mzima,” .
“Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, hazifungamani, zipo katika mawimbi, rangi na style za kisasa, ni nyepesi, rahisi kusukia, laini, zinadumu kwa muda mrefu na muhimu kuliko yote zipatikana kwa bei nafuu sana.”
“Ni bidhaa ambazo naweza kusema confidently zinamfaa mwanamke wa kisasa.”
Jokate amesema utengenezaji wa nywele hizo ameusimamia mwenyewe na kwa msaada wa timu yake ya Kidoti.
Categories: , , , ,