TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA SHARO MILLIONEA .


Msanii wa Bongo movie na mwanamziki Hussein Mkieti " Sharo Milionea" amefariki dunia leo hii kwa ajali ya gari alipokua akielekea Muheza, Tanga.

Nukuu from Sammisago=====>
Taarifa kuhusu kifo cha Msanii wa maigizo na Mziki wa Bongo fleva kufariki zimasamba nchi nzima masaa machache yaliopita.Nimepata uthibitisho kutoka kwa diwani Makame Seif ambaye ni rafiki yake wa karibu sana wa Marehemu Hussen Ramadhani Mkiete maarufu kama Sharo Millionea amepata ajali mida ya saa mbili eneo la maguzoni Tanga na amefariki dunia hapo. Polisi wametambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi. Diwani huyu amefahamisha sammisago.com kuwa Sharo millioneea ameumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono. Sammisago.com imezungumza na  Mjomba wa marehemu na amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na Kesho asubuhi ratiba ya msiba itatolewa. Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo imeshafika Hospitali ya Teule.
R.I.P Brother!!