Picha: Kariakoo Kwawaka tena, Mabomu ya machozi yapigwa

Kwa mara nyingine tena leo kumeshuhudiwa machafuko mengine katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya polisi wa FFU kutumia mabomu ya machozi kulitawanyisha kundi kubwa la waumini wa dini ya kiislam waliokuwa wanaonekana kutaka kuandamana.
Pamoja na kutofanyika kwa maandamano, mkusanyiko mkubwa wa waislam nje ya msikiti uliopo maeneo haya baada ya swala ya Ijumaa uliwafanya polisi kutumia jitihada mbalimbali kuutawanyisha na baadhi ya watu kukamatwa na polisi akiwemo sheikh mmoja.Source =====>Bongo5.com

Categories: ,