U HEARD: Uvutaji Sigara Unaozesha Ubongo


Kuvuta sigara kunaozesha ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo wa kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini Uingereza.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50
ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na kiharusi.
Shirikisho la kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha Cholesterol au kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri ubongo.
"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
Kuvuta sigara “kwaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, masomo na uwezo wa kushaurianana, kulingana na wachunguzi wa King’s College, London.
Katika Kupambana na tabia ya Uvutaji sigara katika nchi za Afrika Mashariki
Tanzania wanaharakati waliandamana mbele ya ofisi za jiji la Dar es Salaam na Wizara ya Afya Novemba mwaka jana kuwasilisha madai ya kutaka serikali ichukue hatua kali zaidi katika masharti ya utangazaji wa bidhaa za tumbaku.
Nchini Kenya serikali imechukua hatua kadha kupunguza tabia ya uvutaji ikiwa ni pamoja na kuweka masharti makali katika matangazo ya sigara na bidhaa nyingine za uvutaji na pia kuzuia uuzaji wa sigara moja moja kwa lengo la kufanya tabia hiyo iwe ya gharama kubwa mtu anapolazimika kununua paketi nzima. Hata hivyo, ingawa kuna dalili za upunguaji wa uvutaji wasiwasi upo hasa kwa vijana wanaoanza kuvuta sasa. 
Uganda pia imepiga hatua kubwa katika masharti ya matangazo ya bidhaa za tumbaku lakini uvutaji sigara ungali katika kiwango cha juu.
Imedhihirika pia kuwa idadi kubwa ya wanawake wanavuta sigara tena hadharani kuliko ilivyokuwa katika ya nyuma. 
 


Categories: ,