HII NDIO COVER YA BUM KUBAM DVD YA NIKKI WA II

Documentary ya kwanza ya ya wimbo wa hip hop Tanzania BUM KUBAM DVD inayomhusisha Nikk wa pili, G nako, Bontha na watu wengine maarufu kama Adam mchomvu, sam misago, Millard ayo, Adamu Juma imeingua mtaani kuanzia tarehe 21/12/12. BUM KUBAM DVD itasambazwa kwa mfumo mpya kabisa wa CODE NAMBA uliopewa jina la MFUMO RAFIKI na umeanza kutumika rasmi tarehe 21/12/12 
FAIDA ZA MFUMO RAFIKI

1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo na kuona idadi ya nakala zote alizouza, muda na mahali zilipouzwa.
2. Unazuia wauzaji feki kuuza kazi ya msanii.
3. Msanii atamfahamu kila mtu aliyenunua bidhaa yake na kuwasiliana nae moja kwa moja.
4. Wezi wote wa kazi ya msanii watajulikana hadharani.
5. Kazi ya msanii itapatikana kwa urahisi na kwa wakati.
6. Unapunguza vichocheo vya piracy kwa kiasi kikubwa sana.