Feza Kessy na Ammy Nando ndio wawakilishi wa Tanzania kwenye BBA [The Chase]


Tanzania inawakilishwa na washiriki wawili kwenye shindano la mwaka huu la Big Brother Africa lililopewa jina la ‘The Chase’. Ufunguzi wa shindano hilo umeanza muda huu huko Afrika Kusini. Washiriki hao ni Feza Kessy na Ammy Nando. Feza Kessy ambaye aliwahi kuwa Miss Dar City Centre, na  Ammy Nando yeye ni Model Mtanzania ambae huwa anafanya kazi zake huko Los Angles, California.