Jikubali yaandika historia kwenye career ya Ben Pol na Nisher kwa kuwa video yao ya 1 kuchezwa Channel O

Video ya Jikubali ya Ben Pol imekuwa ya kwanza kuchezwa kwenye kituo cha runinga cha Channel O cha nchini Afrika Kusini tangu mkali huyo wa RnB aanze muziki.
Jikubali  ndio video ya kwanza aliyoiongoza na kuitayarisha Nisher kuwahi kuchezwa kwenye kituo hicho.
“Mimi mwenyewe nimeshangaa maana ndio ya kwanza, kwakweli nimefurahi na zaidi namshukuru Mungu na pia nawashukuru pia watu ambao wamejaribu kutumia nguvu yao binafsi kama Lucci, Nisher akina Jokate,”Ben Pol ameiambia Bongo5.
Ben Pol amesema awali aliwahi kupeleka video zake mbili za Samboira na Maneno lakini hazikuweza kukidhi viwango vinavyotakiwa kuwepo kwenye video zinazochezwa Channel O.
“Nimewahi kupeleka kama yatima huna hata mtu unamjua unayeweza kumuuliza hata video imefikia wapi.”
Kwa upande wake Nisher amesema tarehe ya leo ni muhimu sana katika maisha yake na ana furaha isiyo na mfano.
“Hakuna video yangu hata moja imewahi kufika mbali kwa kiwango hicho,”amesema Nisher.
“Nimewahi kuwa na ndoto kwamba ningependa ifike mbali kiasi hicho lakini sikuwahi kujua itafanikiwaje. Kwa siku kama ya leo yaani nafurahi, hii tarehe naenda kuiandika sehemu.”
“Kuna watu wenye majina makubwa ambao wananiamini sana kwenye kazi ninazofanya na wamenisupport, shout out to Jokate, shout to Lucci, shout out to Ben Pol, shout out to anybody anayeona kabisa kwamba kitu ninachofanya kinaweza kufika mbali.”
#Congratulations Ben Pol na Nisher kwa kuvusha Border Muziki wa Tanzania!

Categories: , , , ,