Nyandu Tozi ft. Young Dee, Young Killa & Belle 9 – Kwa Mafans [Audio]


Rapper Hamidu Salim Chambuso aka Nyandu Tozi leo ameachia ngoma yake mpya aliyowashirikisha Young Killa, Young Dee na Belle 9 iitwayo ‘Kwa Mafans’. Kwa Mafans imetayarishwa kwenye studio za Classic Sounds chini ya producer Mona G.

Nyandu amesema ameamua kuwashirikisha Young Dee na Young Killa kwakuwa licha ya umri wao mdogo, vijana hao wana vipaji vya hali ya juu kwenye uandishi wa mashairi ya hip hop na maisha yao yote yamezungukwa na muziki.
Pia amesema amefanya wimbo huo na Mona G kwakuwa ni producer anayefahamiana naye kitambo na ndiye aliyeproduce wimbo wake uliopita, Nimekasirika (Mona aliingiza sauti na kufanya final mixing huku beat ikitengenezwa na Marco Chali) na kusisitiza kuwa anakubali uwezo wake katika utengenezaji wa nyimbo.
Nyandu ameiambia Bongo5 kuwa Jumapili hii (July 7) itakayokuwa siku ya birthday yake, ataizindua rasmi ngoma hiyo na kusindikizwa na Young Killa, Young Dee, Chidi Benz, Country Boy, Mirror na wengine. Amedai kuwa muigizai wa filamu Wema Sepetu atakuwepo kuikata keki ya birthday.